Chocolate & coconut Tosca cake
VIPIMO:
200 g siagi
4 mayai
5 cups sukari
2 vanilla sugar (kijiko cha chai)
1 cup cocoa
3 cups unga wa ngano
Glaze:
200 g (5-6 vikombe) desiccated coconut (machicha ya nazi) 1 cup cha syrup 2cups vya sukari 5/1cup Cream 75 g siagi
Maelekezo:
1:washa jiko lako, joto la 200
2:Yayusha siagi kisha changanya na sukari, saga mpaka sukare iyayuke.
3:Kisha weka mayai, changanya vizuri na baadae weka vanilla suger, cocoa pamoja na unga. changanya vizuri mpaka vitu vyote vichanganyike vizuri
4:Chukua chombo cha kuchomea na upake siagi kwandani, mimina keki yako na uichome kwa muda wa dakika 15-20
NAMNA YA KUANDA GLAZE:
1:Changanya machicha ya nazi,sukari,siagi,fresh cream na syrup katika sufuria kisha weka jikoni, moto mdogo mdogo
2: Ichanganye changanye vizuri na uiache ichemke kwa muda wa dakika 3-5
Keki yako ikishaiva, itoke kwenye oven na umwagie glaze kwa juu, kisha uisambaze vizuri (ifunike kike yote) baada ya hapo utairudisha keki yako kwenye oven na uichake kwenye oven kwa muda wa dakika 10 iliiweze kubadilika rangi (golden brown color)
Baada ya hapo utaitoa keki yako kwenye oven na kuiacha ipoe, ikiashapoa utaikata kata vipande upendavyo na itakua tayari kwa kuliwa