Vitumbua
Vipimo:
Mchele 2 mugs
Tui la nazi 2 mugs
Yai 1 kubwa
Sukari ½ mug
Hiliki ½ kijiko cha chai
Hamira ½ kijiko cha chai
Unga wa ngano 2 vijiko vya chakula
Samli ya kupikia (au mafuta) kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1:Osha na roweka mchele masaa 6 au usiku mzima
2:Saga mchele na tui kwenye mashine ya kusagia (blender) mpaka uwe laini usiwe na chenga.
3:Tia hiliki, hamira na unga wa ngano saga tena mpaka uchanganyike.
4:Mimina kwenye bakuli na uache uumuke kiasi.
5:Ukisha kuumuka changanya sukari na yai
6:Tumia kama kijiko 1-2 cha chai cha samli kwa kukaangia kila kitumbua.
7:Mimina mchanganyiko kiasi kwenye kikarai maalumu cha kuchomea vitumbua
8:Kitumbua kikiiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka kiwe tayari.
9:Panga kwenye sahani. unaweza kula vitumbua vikiwa moto au vikipowa.
http://alhidaaya.com/sw/node/3041