top of page

Mchicha wa Nazi


mchicha wa Nazi

Mahitaji:

Mfuko 1 wa mchicha

Karoti 1

Kitungu 1

Chumvi kiasi

Tui la nazi kiasi

Hoho 1(kijani,njano au nyekundu, haijalishi)

Upikaji:

1: Osha mchicka na ukatekate upendavo

2: Weka mchicha kwenye chombo cha kupikia, kisha weka kitungu, hoho, karoti na chumvi.

3: Weka jikoni na ufunike, Pika mpaka utakapoona mchicha umeanza kujitoa maji na kukauka kiasi.

4: Weka tui na uendelee kupika mchicha kwa muda kidogo

5:Toa mchicha jikoni na baada ya hapo utakua tayari kwa kuliwa

Mchicha wa nazi unaweza kuliwa na Wali, Ugali, Mkate n.k

Obs!

sikutaka mboga yangu iwe na michuzi michuzi kwahiyo nilitumia nazi kidogo tu na pia hoho nilitumia hoho za rangi mbili, ya njano na nyekundu


bottom of page