top of page

Bata wa kuchoma


Mahitaji

8 servings

Bata 3kg:

Vitu vya kujaza ndani ya bata

Vitungu vyekundu 3

Thyme kijiko 1 cha chakula

Rosemary kijiko 1 cha chakula

Sage kijiko 1 cha chakula

Kitungu swaumu

Tangawizi

Limao 1-2

Mchanganyiko wa kupala juu

Soya ya kichina/kijapani (Kiasi)

Siagi iliyoyajushwa 50-80g

chumvi na pilipili manga

Kwenye chombo cha kuchomea

Maji 2cup

Vitungu vyeupe 2

karoti 2

Prunes vitunda 5

Naman ya kupika:

1: Msafishe Bata na akikisha hana majimaji

2: Changanya swaumu,tangawizi, thyme,rosemary,sage,chumvi pamoja limao

3 :Mpake Bata viungo kwa ndani na kisha utamalizia kwa kuweka Vitungu (kata vitungu mara mbili)

4 :Changanya soya,siagi,chumvi na pilipi kisha umpake Bata kwa juu (mpake viungo kote)

5 :Weka Bata kwenye chombo cha kuchomea na umuweke kwenye oven, moto wa 225 kwa muda wa dakika 30

6 :Mtoe Bata na upunguze moto mpaka 175

7 :Weka maji,kitungu,karoti na prunes pembezoni mwa Bata. Mrudishe Bata kwenye oven na uendelee kumchoma (mgongo wake ukiwa juu)

8 :Mgeuze bata baada ya masaa 2 kisha umnyunyuzie siagi iliyoyayushwa, pungunza moto mpaka moto wa 140. Lisaa 1 baada ya hapo Bata atakua tayari amewiva na tayari kwa kuliwa.

Obs!!!Utamuacha apoke kwanza, mimi niliweka na viazi pamoja na nyanya ndogo ndogo. Vitungu nilikata mara mbili, unaweza pia kuweka vipande vya apple ukipenda


bottom of page